SALMA MKALIBALA, MASASI

mtwarapressclub@gmail.com

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ameonya juu ya mila na desturi kandamizi zinazofanywa kwa watoto wa kike zinazopelekea kuwakosesha nafasi ya kupata elimu.

Rais Samia amesema hayo Septemba 17, 2023 wakati akiongea na wananchi kwenye uwanja wa Boma, uliopo Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara akiwa aahitimisha ziara yake ya siku nne mkoani Mtwara.

Aidha Dkt. Samia amewataka wazazi na walezi kutumia pesa wanazozipata kwenye  mavuno kupitia mazao mbalimbali kukuza uchumi wa vipato vyao badala ya kuendekeza mila hizo.

Amesema anazo taarifa za wakazi wa maeneo hayo kufanya sherehe za mara kwa mara kwa ajili ya kuwacheza Watoto wao badala ya kujikita kuweza katika kujiletea maendeleo.

‘’Sisemi tuache….. kwa sababu ni mila zetu, twende nazo lakini tupunguze mambo ya kuwacheza wasichana wakiwa wadogo kisha mnampa ruhusa ameshachezwa nenda tuyaache, haya haiwajengei wazingira vizuri’’

‘’Wasichana wetu wachezeni wakiwa na umri wa kujua wamechezwa na wameyaelewa waliyochezwa nayo lakini sio wakiwa wadogo alafu mnaawachia mna uhuru nenda haya yanatuharibia, mimba hizi ndiko zinakopatika” amesema

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Mtwara iliyoanza Septema 14, 2023 na kuelekea Mkoani Lindi.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…