MWANDSIHI WETU, PWANI
mtwarapressclub@gmail.com
Wakulima wa Zao la Ufuta Kata ya Nyamato Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani wameipongeza taasisi ya utafiti wa kilimo Tanznaia TARI Naliendele kwa kuwwapatia mbegu bora zinazostahimili ukame hali ambayo imepelekea ufuga kumea vizuri katika mashamba yao licha ya kuwa na uhaba wa mvua.
Akizungumza katika mashamba tofauti kwenye eneo hilo hivi karibuni, Ofisa Ugani Kilimo Kata ya Nyamato Ami Said Jesi amesema kuwa walipewa mbegu kwaajili ya mashamba darasa mbegu aina tatu kisha kupewa mbegu za kienyeji ambapo zilipandwa zote na zote zimeota licha ya kutokuwa na mvua.
Ameeleza kuwa wakati wa maandalizi ya shamba walipokea mbegu kutoka TARI kwa ajili ya kuandaa shamba darasa utaratibu ambao  unaweza kuongeza hamasa kwa kulima zao hilo.
“Tumepanda mbegu zote ambapo zinaonyesha hazijafanya vizuri kutokana na kutokuwa na mvua  lakini pia wakulima wangu wanahitaji elimu zaidi ili kupata ufahamu zaidi namna ya kupanda, aina za mbolea tunazopaswa kutumia pia namna gani bora ya kuondoa magonjwa na wadudu wasumbufu wa mazao”
kwa upande wake Mratibu wa Program ya zao la Ufuta Kitaifa Joseph Nzunda amesema walitoa aina hizo ili kutoa nafasi kwa mkulima kujifunza zaidi na kuchagua mbegu gani inamfaa.
“Yaani aina zote nne za mbegu tumepanda maeneo mengi ya Wilaya hii na inaonekana kufanya vizuri hata ufuta unakubali tunahitaji kuendelea kutoa elimu namna ya kupanda idadi ya mimea namna ya kupanda mimea shambani”
“Yapo maeneo mengi nchini ambayo ufuta unaweza kustawi wananchi wahamasike kulima zaidi tukilima kwa wengi tuwe
Naye Gasper Mgimiloko kutoka Kitengo cha Uharishaji wa Teknologia na Uharishaji anasema kuwa kutokana na wananchi wengi kuitikia kulima zao hilo kitengo hicho kitatumia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata elimu sahihi juu ya zao la ufuta.
“Tunapita kuangalia mashamba ya mfano ambayo yamepandwa katika mkoa wa pwani ambapo tunaona yanaenda vizuri tunaimani kuwa yataongeza hamasa kwa wakulima kulima zaidi zao la ufuta”
Kwa upande wake Ofisa kilimo msaidizi kutoka Tari Naliendele Nicko Lukoya anasema kuwa wakulima wawasikilize  na kufuata maelekezo ya wataalamu ili waweze kulima kilimo bora chenye tija kwao.
“tunaona shamba wamelima vizuri wamepalilia na kuweka dawa za kudhibti wadudu tunawashauri waendelee kutumia mbolea za maji na dawa za kuua wadudu ili kuwadhibiti”
“Kupitia hapa tunaweza kushawishi wakulima kubadilika na kuchukua tekenolojia hii na kuipeleka katika mashamba yao ili kuongeza uzalishaji wa ufuta zaidi” alisema Lukoya

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…