BRYSON MSHANA, MTWARA
Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), imetangaza rasmi ratiba ya Korosho Marathon msimu wa nne, ambayo mwaka huu inatarajiwa kufanyika tarehe 29 Novemba 2025 na kushirikisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari leo tarehe 10 Octoba 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Francis Alfred, imeeleza kuwa Korosho Marathon ya msimu huu imeboreshwa na inatarajiwa kuwa ya kipekee tofauti na misimu iliyopita.
Kwa mujibu wa Alfred, Korosho Marathon ya msimu huu itajumuisha maonesho ya bidhaa na shughuli mbalimbali zinazohusiana na zao la Korosho, lengo ikiwa ni kutoa fursa kwa wananchi kujifunza na kufurahia thamani ya zao hilo kuu la Uchumi katika Mikoa ya Mtwara na Lindi.
“Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Korosho Marathon, tukio hili litakwenda sambamba na Maonesho ya Bidhaa za Korosho, yatakayofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 29 Novemba 2025, katika viwanja vya fukwe za Millennium, Mtwara,Maonesho haya yatatoa nafasi kwa wakulima, wajasiriamali, wawekezaji na wanunuzi wa ndani na nje ya nchi kujionea ubunifu na thamani ya mnyororo wa bidhaa zitokanazo na zao la korosho”.
“Kama ambavyo tumekuwa tukifanya miaka yote, lengo kuu la Korosho Marathon ni kuhamasisha jamii kuhusu ulaji wa Korosho, kuelezea fursa zinazopataikana kupitia zao hilo, pamoja na kuhamasisha umuhimu wa afya bora inayotokana na kula korosha sambamba na kuboresha michezo nchini” amesisitiza Alfred
Ameongeza kuwa malengo makuu ya Korosho Marathon ni kukuza na kuhamasisha matumizi ya korosho na bidhaa zitokanazo na korosho ndani ya Tanzania, uuongeza uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa sekta ya korosho katika uchumi wa taifa, kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mikoa ya kusini (Mtwara, Lindi, Ruvuma) na kukuza afya na kuendeleza utamaduni wa mazoezi katika jamii ya Watanzania.
Ameelezea upekee mwingine wa mbio za mwaka huu kuwa ni kuhusika kwa watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 13 watakaokimbia umbalia wa 2.5 km na zile za wazee wenye umri wa miaka 60 hadi 15, ikiwa ni sehemu ya kutoa nafasi ya watu wa rika zote kushiriki.
Naye mesmaji wa Korosho Marathon 2025 Mohamed KemKem, amewataka washiriki kujiandaa mapema kuanzia kwenye maonesho kwa ni wakati wao kuonesha upekee wa bidhaa za Korosho, na pia kutoa nafasi kwa jamii kujiweka vizuri kiafya.
“Tunatoa rai kwa wadau wote – taasisi binafsi, za serikali, washirika wa maendeleo, mashirika ya michezo na afya, pamoja na wananchi kwa ujumla, kushiriki kikamilifu katika maandalizi na ushiriki wa tukio hili kubwa la Korosho Marathon 2025” amesema
Kaulimbiu ya Korosho Marathon 2025 ni “Eat Cashew, Be Heath” huku gharama za usajili zikiwa Shilingi 35,000 kwa watu wazima na 20,000 kwa watoto.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






