BRYSON MSHANA, MTWARA
Ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali Mkoa wa Mtwara, imefanya kikao cha kwanza cha Kamati ya ushauri wa kisheria, chenye lengo la kupeana majukumu na namna ya utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na ushauri na uangalizi katika utekelezaji wa huduma za ushauri wa kisheria na Elimu ya Sheria kwa wananchi.
Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mtwara, leo tarehe 12 Septemba 2025, na kufunguliwa na Wakili wa serikali Mkoa, Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali Nunu Mangu.
Kwa mujibu wa wakili Nunu Mangu, kamati hiyo imeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Utekelezaji wa Majukumu, Huduma ya Ushauri wa Kisheria za Mikaoa na Wilaya, vidokezo vya Mwaka, 2024).

“Lengo kuu la kamati hii ni kuwezesha Mawakili wa Serikali kuhakikisha utawala wa sheria unafuatwa na kutekelezwa katika Mikoa na Wilaya kwa minajili ya kupunguza migogoro ya kisheria dhidi ya serikali”
Kikao hiki cha kwanza kina umuhimu wa kipekee, kwani pamoja na kujitambulisha tunatarajia kujadili majukumu ya kamati, kupanga mikakati ya utekelezaji, na kujenga msingi thabiti wa ushirikiano kati ya kamati na viongozi wa serikali na wadau wengine katika kutoa ushauri, msaada wa kisheria, elimu na uelewa kwa viongozi, watumishi wa umma na umma kwa ujumla juu ya umuhimu wa kufuata sharia” ameeleza Wakili Nunu.
Amewakumbusha wajumbe wa kamati hiyo kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia Weledi, Uadilifu na Uzalendo mkubwa huku wakitanguliza mbele maslahi ya Mkoa na Taifa kwa ujumla kwa kuzingatia kuwa haki ni msingi wa mani, maendeleo na mshikamano wa kijamii.
Mjumbe wa kamati hiyo wakili wa serikali Naftal Mzava ameeleza kuwa wamejipanga vema kwenda kuwatumikia wananchi, kwa kuhakikisha kuwa wanapata msaada, ushauri na elimu ya masuala ya kisheria ili kujenga jamii iliyostawi.
“Kama ambavyo mmesikia, hiki ni kikao cha kwanza na kamati hii inalenga kutoa usaidizi katika ofisi za serikali ili kutatua migogoro ambayo ilikuwa inawawia vigumu watendaji mbalimbali kuitatua na kupata suluhisho” amesema Mzava.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






