BRYSON MSHANA, LINDI
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kukamilika kwa mradi mkubwa wa uchakataji na usindikaji wa gesi asilia ya kimiminika (LNG) mkoani Lindi, mradi ambao umesimama kwa zaidi ya miaka 12.
Akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika Lindi Mjini, Dkt. Samia alisema Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo na mwekezaji, hatua itakayofungua njia ya kusainiwa mikataba na hatimaye kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo.
“Natambua kiu yenu kubwa na ya Watanzania kwa ujumla ni kuona mradi wa gesi asilia ya kimiminika, yaani LNG wa kule Mchinga. Tumekuwa na mizunguko ya mazungumzo ndugu zangu kwa miaka miwili, sasa tunakaribia kukubaliana, tupo hatua za mwisho,” alisema.
Mradi huo unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 40 (zaidi ya Sh70 trilioni) na unatarajiwa kuleta ajira zaidi ya 13,000 za moja kwa moja, sambamba na kuchochea ukuaji wa uchumi na vipato vya wananchi wa Lindi na Taifa kwa ujumla.
Dkt. Samia alisisitiza kuwa mazungumzo yamekuwa ya kina kwa kuzingatia manufaa ya pande zote mbili – mwekezaji na Serikali. “Anayewekeza lazima awe na uhakika wa fedha yake itamzalishia nini. Lakini na sisi pia lazima tuwe na uhakika mradi huu unainufaisha nchi na wananchi wake,” alisema.
Hakikisho hili linakuja wakati ambapo Watanzania, hususan wakazi wa Lindi, wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu hatua ya mwisho ya utekelezaji wa mradi huo unaotajwa kuwa wa kihistoria katika sekta ya nishati nchini.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






