BRYSON MSHANA, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameonesha kushangazwa na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara, kwa kushindwa kutumia fedha za mapato ya ndani kujenga jengo kwa ajili ya kuweka mashine ya Miyonzi (X-Ray) katika kituo cha afya kata ya Chiwale.
Akizungumza na wananchi wa Masasi katika mkutano wa hadhara Septemba 17, 2023 ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara, Dkt. Samia ameeleza kuwa Halmashauri kupitia mapato yake inao uwezo wa kujenga jengo hilo badala ya kuitegemea serikali kwa kila kitu.
Rais Samia alikuwa akitolea ufafanuzi hoja iliyowasilishwa nna Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe, aliyeeleza changamoto ya ukosefu wa jengo hilo licha ya serikali kupeleka mashine hiyo ya X-Ray.
“Hivi kweli Halmashauri kama kweli mnataka hii mashine ihudumie watu, mnashindwa kupata Mil. 250/300 kujenga jengo ambalo hii mashine itawekwa na kuweza kuhudumia wananchi, yani kila kitu kila senti itoke serikali kuu, hamko ‘serious’ hamko ‘serious’ kabisa na maendeleo ya watu.”
“Mmejilemaza, mmejilemaza tulisema asilimia 40 ya mapato ya kila halmashauri yaelekezwe kwenye shughuli za maendeleo.” Amesema Dkt. Samia.
Kufuatia hali hiyo, Dkt.Samia amewataka watendaji wa halmashauri na madiwani kujitizama upya na kutafta fedha shilingi Milioni 300 kwa ajili ya kujenga jengo hilo.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Mtwara iliyoanza Septemba 14, 2023 na kuelekea Mkoani Lindi.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






