BRYSON MSHANA, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka watanzania kuzingatia amani na utulivu wakati wanapojiandaa kwa ajili ya uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Rais Dkt.Samia ametoa Rai hiyo Septemba 15, 2023 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Nangwana Sijaona Mjini Mtwara, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoai Mtwara iliyoanza Septemba 14, 2023.
Dkt. Samia ameeleza kuwa tayari watu wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali wameshaanza kufanya maandalizi ikiwepo kwenye majimbo, hivyo wajitahidi kuhakikisha kuwa wanazingatia utu, heshima na ubinadamu wakati wote wa kutafuta nafasi za uongozi.
“Kujipanga kwenu kwa ajili ya Uchaguzi kusije kuharibu Amani na Utulivu wa Nchi yetu, hakuna haja ya kuwa na ugomvi, Kila aliyefanya kazi vizuri wananchi wamemuona na watamrudisha katika nafasi yake hivyo kila mmoja azingatie.
“Tufanye Uchaguzi kwa kuheshimu mila na destiri zetu, tujue kuwa Demomrasia sio kutoa lugha za matusi kwa wengine, tujitahidi kuongea kwa heshima na kuheshimiama”amesisitiza Rais Dkt. Samia.
Aidha Mhe.Rais Dkt.Samia ameeleza juu ya kila mtanzania kupata maendeleo bila upendelea na kusisitiza kuwa Demokrasia ni pamoja na kuhakikisha kuwa watu wote wanafikiwa na maendeleo yanayoletwa na serikali katika maeneo yao.
“Tusitimie Demokrasi kuwakosesha watu maendeleo, Demomrasia ni kukuza Maendeleo na Sio kufifisha Maendeleo, tunaposhusha Fedha za Maendeleo ziende kufanya kazi na sio kusema huku kuna nani huku kuna wakina nani watu wote wanataka maendeleo” ameongeza Dkt. Samia
Rais Skt. Samia Suluhu Hassan yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku nne itakayohitimisha Septemba 17, 2020 ambapo Septemba 15, 2023 alikagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, ikiwepo kuzindua rasmi Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini, kutembelea Bandari ya Mtwara, Uwanja wa Ndege Mtwara pamoja na kuzindua Barabara ya Mtwara – Mnevata yenye urefu wa Kilomita 50 iliyojengwa kwa kiwango cha Lami.
Ziara hii pia itamfikisha Rais Dkt Samia katika Wilaya za Tandahimba, Newala, Masasi pamoja na Nnanyumbu ambako akiwa katika maeneo hayo atapata nafasi ya kuendelea kukagua miradi mbalimbali, kusalimia wananchi pamoja na kufanya mikutano ya hadhara.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






