SALMA MKALIBALA, MASASI
mtwarapressclub@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi nchini kurekebisha udhaifu wa kimahusiano uliopo baina ya viongozi mbalimbali na watendaji wa serikali ili wapeleke maendeleo kwa wananchi.
Rais amesema hayo Septemba 17, 2023 wakati akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Masasi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika uwanja wa Boma, ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Mtwara iliyoanza Septemba 14, 2023.
Amesema viongozi wamewekwa katika nafasi mbalimbali ili wapeleke maendeleo kwa wananchi, na si kujali na kuthamini maendeleo yao kwanza na ya wananchi baadaye.
Ameeleza kuwa kukosekana kwa mahusiano hayo kunaweza kuchangiwa na viongozi hao kutaka kuonekana wabora zaidi kuliko wenzao au kuwa na mivutano binafsi baina yao.
“tumewaweka katika kazi mbalimbali ili mtizame maendelea ya wananchi, hatukuwaweka mtazame maendeleo yenu kwanza, ya wananchi baadaye, Hapana mpeleke maendeleo kwa wananchi”
Wajerumani wanamsemo wanasema, Samaki akioza anaanza kichwani, ukimtizama Samaki kichwani hayuko vizuri, Samaki wote huyo hayupo vizuri, sasa kama hakuna uhusiano baina ya watendaji na viongozi katika eneo ili na kiongozi maana yake ni kuongoza njia, kiongozi ni kuongoza njia, kama mtendaji hayuko vizuri unamuongoza akae vizuri, sasa kulalamika hapa uhusiano wa watendaji na viongozi, ebu viongozi mjitazameni vizuri” amasema
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






