MWANDISHI WETU, NAKONDE
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Tanzania Dkt. Hashil Abdallah na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia Bi. Lillian Bwalya wamesaini nyaraka za makubaliano za kuondoa changamoto za kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Makatibu Wakuu hao wamesaini nyaraka hizo za makubaliano (Communique) katika Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu wakati wa Mkutano wa Pili wa Pamoja wa Kujadili Changamoto za Biashara baina ya nchi hizo uliofanyika katika Mpaka wa Nakonde – Zambia Novemba 07, 2023
Vilevile Dkt. Abdallah amesema utatuzi wa Changamoto hizo utaiwezesha sekta binafsi kaika nchi zote mbili kufanya biashara kwa urahisi na tija hususani katika biashara ya huduma ya usafirishaji mizigo kutoka Tanzania kupitia Zambia na kwenda nchi nyingine na mizigo kutoka Zambia kupitia Tanzania kwenda nchi nyingine.
Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia Bi Lillian Bwalya amesema nchi hizo zitaendelea kushirikiana katika kitatua changamoto hizo pamoja na nyingine zitakazojitokeza ili kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa pande zote mbili.
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






