OR-TAMISEMI

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaaa Mohamed Mchengerwa, amesema Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imepiga hatua kubwa katika kuleta maendeleo na kufanya mapinduzi ya kiuchumi katika Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo Novemba 22, 2023 Jijini Dar es Salaam, wakati akiwa katika mahojiano maalumu na kituo cha Televisheni cha Clouds kupitia kipindicha 360.

Akizungungumzia Jimbo la Rufiji ambalo yeye ni Mbunge, Mchengerwa mmesema mapinduzi hayo yameweza kubadilisha fikra za wananchi hali ambayo imesababisha mapokeo chanya na imani ambayo wananchi wameijenga kwa Serikali na Rais Dkt. Samia.

“Rufiji kulikuwa na kilio cha wananchi katika maeneo mengi ikiwepo suala la barabara, na kwa kipindi cha miaka miwili ujenzi wa barabara ya Nyamwage – Utete umeanza na naendelea khuku serikali ikiwa imeweka izaidi ya bilioni 45 kukamilisha mradi huo”

“Rufiji wamepita Wabunge 9 na ilifika wakati Mbunge anaongoza kwa kipindi cha miaka mitano tu kisha anaondolewa ambapo moja ya sababu kubwa ilikuwa ni kilio chao juu ya barabara ya Nyamwage – Utete yenye urefu wa takriban kilomita 33.7 ambayo sasa inatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 18” ameeleza Mchengerwa.

Ameitaja barabara nyingine Ikwiriri – Mkongo ambayo mkandarasi anaendelea na ujenzi wa kiwango cha lami, sambamba na daraja la Mbambe linalojengwa kwa zaidi ya Shilingi bilioni 10.

“Sisi wananchi wa Rufiji na mkoa wa pawani tunamshukuru sana Mh. Rais kwa namna Serikali yake ilivyoufungua mkoa wa Pwanai, na tayari kuna barabara nyingine iko kwenye mpango ya kutoka Chalize – Mloka – Utete – Nyamwage ambayo itawasaidia pia wananchi wa mikoa ya kusini” amesisitiza Mchengerwa

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…