BRYSON MSHANA, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Kamati za Usimamizi wa Maafa ngazi za Wilaya na Mkoa, zimetakiwa kujiandaa kikamilifu kukabiliana na maafa iwapo yatajitokeza, kufuatia uwepo wa Mvua za Elnino zilizotabiriwa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Nchini (TMA).

Maelekezo hayo yametolewa Novemba 22, 2023 na  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga, wakati anafungua mafunzo ya kuzijengea uwezo kamati hizo, yaliyoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

“La kwanza ni kuainisha na kuandaa rasilimali za kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa endapo yatatokea kwa kila sekta kushiriki kikamilifu katika eneo lake.” Amesema Naibu Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuona haja ya kufanyika kwa mafunzo hayo kwa kamati hizo za usimamizi wa maafa ndani ya Mkoa wake, akieleza kuwa yamekuja wakati muafaka.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni Kanali Selastine Masalamado, ameeleza kuwa zipo hatua mbalimbali za kupambana na maafa ikiwa ni pamoja na hatua ya kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na mwisho ni kurejesha hari baada ya kujitokeza kwa maafa.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…