BRYSON MSHANA, MTWARA
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda amewasisitiza wakulima wa Korosho kujitahidi kuzingatia ushauri unaotolwa na wataalam kuhusu namna ya kutunza Koroshi ili zibakie kwenye ubora na kuendelea kuvutia wanunuazi.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo Novemba 10, 2023 wakati akizungumza na wakulima wa zao la Korosho katika Kijiji cha Mkahara Halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara,kwenye Mnada wa nne wa kuuza Korosho uliosimamiwa na Chama Kikuu cha Ushirika MAMCU Ltd.

Baadhi ya wakulima wa Korosho waliowawakilisha wenzao kufungua barua zilizowasilishwa na wanunuzi kuomba kununua Korosho kwenye mnada uliofanyika katika Kijiji cha Mkahara Halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara Novemba 10, 2024 (PICHA NA JUMA MOHAMED)
Katika salam zake kwa wakulima, ameeleza kuwa utunzaji mzuri wa Korosho utaendelea kulipa thamani zao hilo na kuzidi kuvutia wanunuzi kutoka maeneo mbalimbali Duniani, jambo ambalo litazidi kuongeza kipato kwa wakulima na kukuza uchumi wa Taifa.
“Tumekubaliana na wenzetu wa Bodi ya Korosho Tanzania kuwa wakulima waendelee kuelimishwa juu ya utunzaji wa Korosho, lakini pia vyama vitakavyobainika kupokea Korosho zisizo na ubora vichukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kuvizuia kupokea Korosho”
“Wakulima tuendelee kuitunza Korosho yetu ili iendelee kuwa bora na kuzidi kuvutia wateja, tufuate kanuni za kitaalam kupitia elimu inayoendelea kutolewa, na vyama vya msingi viendelee kusimamia ubora” amesema DC Munkunda.
Aidha mkuu wa Wilaya amewataka viongozi wa vyama vya msingi kuharakisha malipo kwa wakulima wa korosho, ili yalipwe kwa na wananchi wapate fedha kwa ajili ya kununulia mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula na kuwaandaa watoto kwa jili ya kujiunga na shule mapema Januari 2024.
“Tumesikia haoa kuwa Wanunuzi walionunua Korosho wanaendelea kufanya malipo kupitia vyama vyenu vya ushirika, niwaombe viongozi wa vyama kuharakisha malipo hayo yawafikie wakulima kwa wakati ili waweze kuendelea na shughuli zao zingie”
“Pia niwaombe tu wakulima kutumia vizuri malipo wanayoyapata ili yaweze kuwasaidia katika kufanya shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kupeleka watoto wao shule” amesisitiza Mkuu wa Wilaya
Zaidi ya Tani Elfu 6.5 za Korosho zimeuzwa kwenye mnada huo, ambao ulihusisha jumla ya Kampuni 30 zilijitokeza na kuwasilisha maombi ya kununua Korosho Ghafi katika Maghala mbalimbali yaliyopo Masasi, Nanyumbu na Mtwara kwa bei ya juu ya Shilingi 2,000/= na bei ya chini shilingi 1,850/=.
Awali akitoa taarifa yam nada huo kwa wakulima, Meneja wa MAMCU Biadia Matipa, alieleza kuwa hadi kufikia jumatano Novemba 8, 2023 Chama Kikuu kilikuwa kimepokea Kiasi cha Kilo 8,342,102 za Korosho ambazo zote zimepelekwa sokoni.
“Tunaendelea na Minada yetu na leo tupo kwenye mnada wa nne, Tayari tulishafanya minada mitatu kwa mafanikio makubwa na kuuza jumla ya Tani 32,538 za Korosho ambazo zimeingiza kiasi cha fedha Shilingi Bilioni 64, 814 ambacho kimeenda kwa wakulima” amesema Bi Matipa.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






