BRYSON MSHANA, TABORA
Timu ya mpira wa Kikapu Wasichana ya Mkoa wa Arusha, imeibuka Bingwa katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) yanayofanyika Mkoani Tabora, baada ya kuwafunga majirani zao Kilimanjaro kwenye mchezo wa Fainali.
Fainali hiyo ya kuvutia ilichezwa Saa 9 Alasiri ya Tarehe 24 Juni 2023, kwenye uwanja A wa Mpira wa Kikapu uliopo Shule ya Sekondari Wavulana Tabora, na Arusha kuifunga Kilimanjaro Jumla ya Vikapu 59-38.
Arusha ni Bingwa mtetezi wa kikapu katika mashindano ya UMISSETA kufuatia Ubingwa ilioubeba mwaka 2022, na imefanikiwa kutetea taji hilo kwa mwaka huu wa 2023.
Katika mchezo mwingine wa fainali ya kikapu Wavulana, Mkoa wa Dar es salaam umeteta ubingwa wake baada ya kuifunga Mwanza kwa jumla ya vikapu 87-76 katika mchezo uliokuwa wa upinzani mkali.
Mchezo huo pia ulichezwa Tarehe 24 Juni 2023 Saa 10 Jioni kwenye uwanja A Shule ya Sekondari Wavulana Tabora, na kuhitimisha rasmi mchezo wa Kikapu kwenye UMISSETA 2023 Mkoani Tabora.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






