BRYSON MSHANA, TABORA
Timu ya mpira wa Miguu Wavulana ya Mkoa wa Geita, imeibuka Bingwa katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) yanayofanyika Mkoani Tabora.
Geita wamewafunga Mabingwa watetezi Mkoa wa Mbeya kwenye mchezo mkali wa fainali uliochezwa katika Uwanja mpya wa Shule ya Sekondari Tabora Wavulana Jumapili Tarehe 25 Juni 2023 Saa 2 Asubuhi.
Mchezo huo ulilazimika kuamuliwa kwa mikwaju ya Penati, baada ya timu zote kwenda Sare ya 1-1 kwenye muda wa kawaida, mbeya wakianza kutangulia na baadae Geita kusawazisha.
Katika hatua ya Penati Geita walifanikiwa kuwazidi Mbeya baada ya kufanikiwa kuingiza langoni Penati 4 huku washindani wao wakipata 3, hivyo fainali kuhitimishwa kwa Geita kuwa Mabingwa wapya wa UMISSETA 2023.
Mchezo wa fainali ulienda sambamba na ule wa kumtafuta mshindi wa tatu katika uwanja A wa Shule ya Sekondari Tabora Wavulana, ukiwakutanisha Mwanza na Rukwa ambao ulimalizika kwa Rukwa kushinda 1-0.
Mratibu wa mchezo wa Soka katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) Erick Mfugale, amesema mashindano ya mwaka huu yalikuwa na upinzani mkali kutokana na timu zote kujiandaa vizuri kuanzia kwa wachezaji mpaka mabenchi ya ufundi.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






