BRYSON MSHANA, TABORA
Mabingwa watetezi wa soka Wavulana Mkoa wa Mbeya, wameingia nusu fainali baada ya kuifunga Dodoma katika Mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) yanayofanyika Mkoani Mtwara.
Mbeya wameifunga Dodoma Magoli 2-1 katika mchezo uliokuwa na upinzani mkali uliopigwa Tarehe 23 Juni 2023 saa 10:00 jioni, kwenye uwanja mpya wa Shule ya Sekondari Wavulana Tabora.
Mchezo Mwingine mkali wa Robo Fainali ulichezwa uwanja A wa Shule ya Sekondari Tabora Wavulana kati ya Mwanza na Lindi, ukimalizika kwa Mwanza kushinda Penati 4-3 baada ya muda wa kawaida kumalizika bila kufungana.
Awali kwenye michezo ya utangulizi Rukwa iliifunga Tanga 1-0, na Kilimanjaro ikaondolewa mashindanoni baada ya kukubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Mkoan wa Geita.
Kwa matokeo hayo Timu za Mbeya, Mwanza, Rukwa na Geita zimefuzu kuingia katika hatua ya nusu Fainali itakayochezwa Tarehe 24 Juni 2023.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






