MWANDISHI WETU, NAKONDE

mtwarapressclub@gmail.com

Katibu  Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Tanzania Dkt. Hashil Abdallah  na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia  Bi. Lillian Bwalya wamesaini  nyaraka za makubaliano  za kuondoa changamoto za kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Makatibu Wakuu hao wamesaini  nyaraka hizo za makubaliano  (Communique) katika  Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu  wakati wa  Mkutano wa Pili wa Pamoja wa Kujadili Changamoto za Biashara baina ya nchi hizo uliofanyika katika Mpaka wa Nakonde – Zambia Novemba 07, 2023

Vilevile Dkt. Abdallah amesema utatuzi wa Changamoto hizo utaiwezesha sekta binafsi kaika nchi zote mbili kufanya biashara  kwa urahisi  na  tija hususani katika biashara ya huduma ya usafirishaji mizigo kutoka Tanzania kupitia Zambia na kwenda nchi nyingine na mizigo kutoka Zambia kupitia Tanzania kwenda nchi nyingine.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zambia  Bi Lillian Bwalya amesema nchi hizo zitaendelea kushirikiana  katika kitatua changamoto hizo pamoja na nyingine zitakazojitokeza ili kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa pande zote mbili.

Check Also

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…