BRYSON MSHANA, MTWARA

www.mtwarapressblog.co.tz

Wazazi na walezi wanaoishi na watoto wenye ulemavu Mkoani Mtwara, wamtakiwa kutowaficha ili kuhakikisha kuwa zoezi la chanjo ya polio awamu ya mwisho linawafikia popote walipo.

Wito huo umetolewa na Mganga mkuu wa Mkoa wa Mtwara Dr.Mohamed Nyembea Disemba 01, 2022 wakati akizungumzia kuanza kwa zoezi la chanjo ya polio awamu ya nne.

Amesisitiza juua ya wajibu wa wazazi kuhakikisha kuwa watoto hao wanapatiwa chanjo kwa awamu ya nne ili wapate kinga ya kutosha ya kuzuia ugonjwa wa kupooza (Polio).

“Watoto 263,883 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hii katika mkoa wa Mtwara, na miongoni mwao tunaamini kuwa wapo wale wenye ulemavu, hivyo tutajitahidi kuwafikia tukishirikiana na wazazi/walezi wao ili kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamili” amesisitiza Mganga mkuu.

Ameeleza kuwa awamu hii ya nne iliyoanza leo Disemba 01, 2022 itakuwa ni ya siku sita na itaanzia majumbani kwa siku nne za mwanzo, na siku mbili za mwisho ni kuwafikia wale ambao hawapo majumbani kama vile mashuleni na maeneo mingine .

Akizungumzia awamu zilizopita, amesema changamoto walioibaini katika kampeni hiyo ilikwa uchache wa siku za kutoa huduma hivyo awamu hii zimeongezeka kutoka siku 4 hadi 6 ili kuwafikia watoto wengi zaidi.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…