MWADISHI WETU, DAR ES SALAAM

mtwarapressclu@gmail.com

Umoja wa Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) wametoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope na mawe yaliyotokea mlima Hanang’ Mkoani Manyara Disemba 3, 2023.

shughuli hii ya kukabidhi msaada imefanyika Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa, ukishuhudiwa na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya ligi Steven Mguto.

Msaada huo umewasilishwa kwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo, Ndugu Dumbaro ili iweze kuwafikia walengwa, ukiwa umeambatana na vyakula, maji,sabuni na vinywaji mbalimbali.

TASWA imetoa msaada huo ukishirikiana na wadau wengine wa michezo nchini, ikiwepo kampuni ya Water Com pamoja na kampuni ya ulinzi ya Bullet Security.

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo, Damas Dumbaro kwa niaba ya Serikali amewashukuru Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania, kwa namna walivyoguswa na kujitolea kidogo walichonacho kwa ajili ya kusimama pamoja na wana Manyara.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…