BRYSON MSHANA, DODOMA
mshanabryson@gmail.com
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeahidi kuendelea kulishughulikia changamoto ya uchumi wa waandishi wa habari na Vyombo vya Habari ambalo limekuwa liklalamikiwa na wadau mbalimbali wa habari nchini.
Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Mobhare Matinyi, wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano mkuu wa umoja wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzania -UTPC Matinyi Desemba 10, 2023.
Amesema Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mawasiliano na Sayansi ya Habari Nape Nnauye ilishaunda kamati maalum ya kufuatililia hali mbaya ya uchumi unaovikabili vyombo vya habari na waandishi wa habari, ambayo tayari imeshakamilishwa kazi yake na iko ikwenye hatua ya kuandaa ripoti ambayo itawasilishwa mwezi January 2024.
“Tayari kamati ile imeshafanya kazi yake kwa kiasi kikubwa, kinachofanyika sasa hivi ni kuiandaa na kuweka vizuri ripoti ambayo itayawasilishwa mwezi januari kwenye mkutano wa wadau wa habari” ameeleza Matinyi.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, rais ya Klabu za waandishi wa habari Tanzania Deogratius Nsokolo, ameiomba Serikali kuendelea kiujenga mazingira wezeshi kwa vyombo vya habari ili viendelee kutekeleza wajibu wao kikatiba wa kutoa habari kwa wananchi.
Nsokolo ameeleza kuwa waandishi wa habari ni sehemu ya Raia wa Tanzania, hivyo wanayo haki ya kulindwa na kuhakikishiwa usalama wao pale wanapokuwa kazini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Keneth Simbeye, amewakaribisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kuunganisha nguvu kwa pamoja na kuwatumikia wananchi kupitia sekta ya habari.
“Tumejipanga kuendelea kufungua milango kwa wadau na kujibidisha ili kuendelea kuzikuza Klabu za waandishi wa habari Tanzania, hali itakayochangia kuwafikia wananchi na kupaza sauti zao kupitia vyombo mbalimbali vya habari”
“Wakati huu ambao tunaendelea na mkakati wetu wa maboresho makubwa ya Taasisi yetu tulioupa kauli mbiu ya “MOVING FROM GOOD TO GREAT” tunahitaji kushirikiana na wadau zaidi na wengine tunawaona hapa mkutanoni, hii ni dalili njema sana”
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






