RAMLA MASALI, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Taasisi ya Joel Nanauka Foundation pamoja na Taasisi ya Africa Success Academy kwa Kushirikiana na Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA )Mkoa wa Mtwara, wameendesha Semina ya Uongozi na Uchumi ikiwakutanisha Maimamu pamoja na Walimu wa Madrasa wakike na wakiume.

Semina hio imefanyika julai 12 katika ukumbi wa Brantaya Manisapaa ya Mtwara Mikindani, lengo likiwa ni kuwapa elimu viongozi wa dini kutokana na kuaminiwa kwao, ambako ni rahisi kufikisha elimu hiyo kwa waumini na Jamii kwa ujumla.

“ moja kati ya hoja zilizoibuka leo ni kwamba elimu hii itolewe kwa Vijana wakiwa wadogo ili wafaidike kwa ajili ya kuongeza tija na kukuza uchumi wa Taasisi zao na kufahamu misingi ya uongozi “ amesema Joel Nanauka Mkurugenzi wa Joel Nanauka Foundation.

Nao washiriki wa Semina hio akiwemo Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania katika Mkoa wa Mtwara Alahaji Mussa Ndazigula amesema Elimu hio kwa ujumla ina manufaa kwa Maimamu na Walimu wa Madrasa kwasababu Kiongozi atajua majukumu ya kuongoza lakini pia kujua namna gani atakuza uchumi.

“ kiongozi mzuri ni yule ambae yupo vizuri kiuchumi kwahiyo tutawafundisha waumini elimu hii ili uchumi wao uwe vizuri” amesema Alahaji Ndazigula.

Naye Bi Bishara Athumani ambae ni Mwalimu wa Madrasa amesema wameelewa kujua namna gani wataweza kukuza uchumi kupitia biashara zao , lakini pia kuwaongoza wenzao bila kwa misingi iliyo bora.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…