JUMA MOHAMED, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Hanafi Msabaha amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo yanayojengwa kwa fedha za BOOST kwenye Shule za Msingi nane zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.

Ukaguzi huo ameufanya Julai 12, 2023 na kuwataka walimu, wasimamizi wa mradi pamoja na mafundi kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa.

Msabaha amezitaka kamati za shule na Ofisi ya Mkurugenzi kuhakikisha wanafanya manunuzi ya vifaa vyote vinavyohitajika kwenye ujenzi katika hatua iliyobaki ili kuharakisha ujenzi wa miundombinu hiyo na ianze kutumika.

Aidha ameiagiza timu ya Menejimenti ya Manispaa kuhakikisha kila siku inakutana kwa ajili ya kujadili maendeleo ya ujenzi wa miradi ya BOOST ili inapotokea changamoto yoyote iweze kutatuliwa mapema.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…