MWANDISHI WETU, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia Hemed Mshamu (74) mkazi wa mtaa wa Rwelu Manispaa ya Mtwara Mikindani, kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa kike wa miaka 10, mwanafunzi wa darasa la Tatu shule ya msingi Rwelu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Mtaki Kurwijila, akizungumza na wanahabari ofisini kwake Novemba 16, 2023, amesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 10, 2023 majira ya saa 10 jioni katika mtaa huo.
“Wakati babu na bibi wa mhanga wakiwa shambani, mhanga huyo alikwenda nyumbani kwa mtuhumia kucheza na ndipo alipohisi usingizi, mtuhumiwa
huyo alimweleza aende kulala kitandani kwake na ndipo alipoingia ndani na kuanza kumbaka hali iliyopelekea kupata mauamivu makali sehemu zake za siri.”
“Mhanga huyo alifikishwa
kituo cha Polisi Mtwara na hatimaye Hospitali ya Rufaa ya Ligula na baada ya vipimo ilibainika ni kweli alikuwa ameingiliwa.” Amesema ACP Kurwijila.
Amesema upelelezi wa tukio hilo umekamilika na kwamba muda wowote jalada litafikishwa ofisi ya Mkuu wa Mashitaka Mkoa wa Mtwara kwa hatua zaidi.
Akizungumzia tukio hilo, mtoto huyo anasema “nikatandika barazani pao, baada ya kutandika mimi nikalala lakini sikulala usingizi, nilifumba tu macho yeye bahati nzuri amepakapaka chokaa akaniambia hivii nenda ukalale ndani, sasa mimi sikuwa na jinsi nikaenda kulala, baada ya kwenda kulala yeye akaja, akaja akanifunua mimi nguo na yeye akamtoa ‘mdudu wake’ akanivua chupi kilichokuwepo ndani akaanza kunibaka..” alieleza mtoto huyo.
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






