MWANDISHI WETU, KATAVI

mtwarapressclub@gmail.com

Mabadiliko makubwa yaliyofanywa na jeshi la polisi, yameelezwa kuwa chanzo cha kupungua kwa vitendo vya ukamatwaji holela wa waandishi wa habari wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kaster Ngonyani wakati akichangia mada katika Mdahalo kuhusu ulinzi na usalama kwa mwandishi wa habari.

Mdahalo uliofanyika Novemba 16, 2023 umeaandaliwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC)kwa kushirikiana na klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Katavi, ambapo ameongeza kuwa jeshi la polisi limefanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji hivyo hakutakuwa na ukamataji wa Waandishi wa habari usiofuata sheria kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Aidha ameahidi kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari na kusisitiza kuwa madhila yaliyowapata wakiwa kazini huenda yalisababishwa na ukiukaji wa maadili kwa askari waliohusika katika matukio hayo.

Naye SSP. Juma A. Jumanne amewataka Waandishi wa habari kuacha vitisho dhidi ya polisi ili kuimarisha mahusiano baina ya pande zote mbili.

“Tukiacha vitisho na ‘victimization’ (kutuhumu) mahusiano na jeshi la polisi yataimarika” amesema SSP. Jumanne.

Mdahalo huo umefanyika katika ukumbi wa St. Matiasi Mpanda Mjini.

Check Also

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…