BRYSON MSHANA, TABORA
Mikoa ya Mwanza na Kigoma imeibuka mabingwa katika mchezo wa riadha mita 100 na 200 Wasichana na Wavulana katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yanayoendelea Mkoani Tabora.
Katika mbio za Mita 100 Wasichana, Aisha Bakari kutoka mkoa wa Mwanza, aliibuka mshindi kwa kukimbia muda wa sekunde 13.44 akifuatiwa na Hawa Dido pia wa Mwanza aliyekimbia sekunde 13.47 na nafasi ya 3 kwenda kwa Admesta Yusuph wa Kigoma aliyetumia Sekunde 13.57.
Kwa upande wa Riadha Wavulana Mita 100, Mkoa wa Kigoma uliibuka bingwa baada ya Alberto T. Alberto kumaliza wa kwanza akikimbia kwa Sekunde 12.03, nafasi ya pili ikienda kwa wenyeji Tabora kupitia Musa Juma aliyetumia Sekunde 12.20 na Mkoa wa Pwani kushika namba 3 baada ya Ally Omary kutumia Sekunde 27.00.
Mita 200 Wasichana kwa mara nyingine Aisha Bakari wa Mwanza aliibuka mshindi kwa kutumia Sekunde 26.66, akifuatiwa na Hawa Dido pia wa Mwanza aliyetumia Sekunde 26.88 na Pelanile Mihumo wa Geita kumaliza wa tatu kwa Sekunde 27.00.
Ama kwa upande wa Mita 200 Wavulana Alberto T Alberto wa Kigoma kwa mara nyingine aliibuka mshindi kwa kutumia sekunde 24.00, huku nafasi ya ikienda tena Tabora baada ya Musa Juma kutumia Sekunde 24.10 na Mkoa wa Dar es salaam kumaliza nafasi ya tatu baada ya Vedastus Raphael kutumie Sekunde 24.60.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






