BRYSON MSHANA, TABORA

mtwarapressclub@gmail.com

Mikoa ya Dodoma na Shinyanga imeibuka mabingwa katika mchezo wa riadha mita 800 na 1500 Wasichana na Wavulana katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yanayoendelea Mkoani Tabora.

Kwa upande wa Wasichana, Angel Tomi kutoka mkoa wa Dodoma, aliibuka mshindi kwa kukimbia muda wa dakika 2.15.90 akifuatiwa na Grace Shija wa Shinyanga aliyetumia dakiaka 1.16.57 na nafasi ya 3 kwenda kwa Zainabu Issa wa Manyara aliyetumia dakika 2.16.63.

Kwa upande wa Wavulana Mita 800, Lemayang Moseka wa Arusha aliongoza na kumaliza wa kwanza akitumia dakika 2.57.81, nafasi ya pili ikienda Dodoma kwa Shukuru Jumanne aliyetumia dakika 2.02.28 na Daudi Kikonywa wa Arusha kushika nafasi ya tatu baada ya kutumia dakika 2.02.31

Katikia mbio za Mita 1500 Wasichana Mkoa wa Tabora uliibuka bingwa baada ya Kashinje Marietha kuongoza kwa kutumia muda wa dakika 4.44.54 akifuatiwa na Grace Shija wa Shinyanga aliyetumia dakika 4.44.85 na nafasi ya tatu kwenda mkoa wa Manyara baada ya Zainabu Issa kutumia dakiaka 4.44.95

Mita 1500 Wavulana Marko Kulaja wa Shinyanga aliongoza kwa kutumia dakika 4.18.56 akifuatiwa na Lomnyaki Kilorit wa Arusha aliyetumia dakika 4.18.98 na nafasi ya tatu kwenda Arusha pia baada ya Lemay moseka kumaliza kwa dakika 4.21.43

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…