BRYSON MSHANA, MTWARA
Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani Mtwara, yamezindua kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili ikiwa ni sehemu ya kuikumbusha jamii juu ya kukemea na kuripoti vitendo hivyo pale vinapotokea katika maeneo yao.
Kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili imeandaliwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mtwara chini ya Mtandao wa MTWANGONET kwa kushirikiana na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mtwara, ikiwa na kauli mbiu ya isemayo “Wekeza Kuzuia Ukatili Wa Kijinsia”
Kampeni hiyo imezinduliwa Novemba 25, 2023 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa Kanal Ahmed Abbas.
Katika uzinduzi huo DC Mwanahamisi amewatoa wito kwa wananchi katika Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara, kutofumbia macho na badala yake wakemee na kuripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyotokea katika maeneo yao.
Ameeleza kuwa vitendo vingi vya ukatili wa kijinsia vinaanza na kuenea katika maeneo watu wanapoishi, hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kuwa anatumia nafasi yake kukomesha hali hiyo ili jamii iendelee kuwa salama.
“Ukiwa kama Mzazi ukiwa kama Mwana jamiii ukisikia mtoto wa mwenzio kalawitiwa au kabakwa ujue pia familia yako haiko salama kwasababu mzunguko huo utazidi kukua” amesema Mkuu wa Wilaya
Mkuu wa wilaya amewaomba wadau yakiwepo mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojishughulisha na kupinga ukatili wa kijinsia, waendelee kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za vitendo hivyo ili kuendelea kuokoa jamii.
Hayo yanajiri wakati baadhi ya tamaduni katika mkoa wa Mtwara kama Jando na Unyago zikitajwa kuwa ni miongoni mwa viashiria vinavyochangia ukatili wa kijinsia, mdondoko wa elimu, pamoja na mimba za mapema.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirka lisilo la kiserikali la FAWOPA ndugu Baltazar Komba ametoa angalizo hilo wakati akitoa salamu kwa niaba ya mashirika mengine 65 yasio ya kiserikali mkoani Mtwara, yaliyojitokeza katika uzinduzi wa siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia.
“Mila hizi zinatajwa mara kadhaa katika tafiti za kitaaluma na makongamano ya kitaaluma na wadau wa maendeleo kuwa zinachochea ukatili wa kijinsia”
“Katika salamu hizi napenda kuwajulisha mkuu wa Wilaya na Waandishi wa Habari kuwa sisi kama mashirika yasio ya kiserikali tulishaanza kuweka mikakati ya kuawafikia makungwi kuwajengea uwezo wa kufahamu mambo gani muhimu yakuwafunza mabinti katika unyago wa kwanza, kwenye ndoa, pamoja na ujauzito.“ amesema Komba.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






