MWANDISHI WETU, MOROGORO

mtwarapressclub@gmail.com

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ametembelea mabanda mbalimbali na kujionea maandalizi yaliofanywa na wadau mbalimbali kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yatakayofanyika kitaifa1 Disemba, 2023 Mkoani Morogoro.

Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo “Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI” yatafanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro ambapo maandalizi ya mwisho yanaendelea.

Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani kitaifa anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa.

Dkt. Yonazi ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza katika maadhimisho hayo na kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI Nchini.

Check Also

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…