MWANDISHI WETU, MANYARA

mtwarapressclub@gmail.com

Kampuni ya Vinywaji ya Bonite Bottlers Limited, imewasilisha salamu zao za pole kwa waathirika wa Maafa ya Mafuriko Hanang kwakutoa mahitaji mbalimbali vikiwemo maji ya kunywa, Unga wa sembe, Mchele, Magodoro pamoja na vitu vingine vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Mil. 50

Aidha, Taasisi ya Arise and Shine chini ya Mchungaji Mwamposa wametoa misaada ya vitu mbalimbali vikiwemo Unga wa sembe, Magodoro kwa waathirika hao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Jenista Mhagama akiambatana na viongozi wengine wa Serikali wameendelea kupokea misaada hiyo.

Waziri Mhagama amemeshukuru Wananchi na Taasisi mbalimbali zinazoendelea kuwasilisha misaada yao kwa waathirika wa Maafa ya Mafuriko Hanang.

Wakati huohuo Serikali imetoa taarifa kuhusu maendeleo ya hali baada ya maafa ya maporomoko ya tope, mawe, magogo na mawe kutoka mlima Hanang Wilayani Hanang Mkoa wa Manyara, yaliyotokea alfajiri ya December 03, 2023.

Taarifa hiyo imesema hadi kufikia saa 6:00 mchana wa leo December 08,2023 idadi ya vifo imefikia 80 (Watu wazima ni 48 wakiwemo Wanaume 19 na Wanawake 29) na Watoto ni 32 (wakiwemo wa kiume 15 na wa kike 17).

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) na Msemaji Mkuu wa Serikali akiongea leo Katesh, Hanang, Manyara amesema “Mwili mmoja wa Mtoto wa kiume ambao ulikuwa haujatambuliwa hadi jana sasa umetambuliwa lakini kuna mwili wa Mwananke mmoja Mtu mzima uliopatikana leo ambao bado haujatambuliwa, hivyo jumla ya maiti zilizokwishatambuliwa hadi sasa ni 79”

“Kwa jumla hadi kufikia saa 6:00 mchana leo December 08,2023 , idadi ya majeruhi waliopokelewa katika Hospitali zetu Mkoani Manyara ilifikia 133 (Watu wazima 71 na Watoto 62, kwa mujibu wa agizo la Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waathirika wote wanatibiwa bure na pia serikali inagharamia mazishi ya waathirika wote”

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…