BRYSON MSHANA, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Chama kikuu cha Ushirika MAMCU LTD, kinachohudumia Wilaya za Nanyumbu, Masasi na Mtwara Disemba 8,2023 kimeendesha mnada wa Nane wa zao la korosho kikipeleka sokoni tani 1,300 na kuuza kwa bei kati ya  shilingi 1,755/= na 1,300/=.

Mnada huo umefanyika katika kata ya Mtawanya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara ambapo takribani kampuni nane zilijitokeza kuomba kununua korosho hizo.

Mwenyekiti wa MAMCU LTD Siraju Mtenguka, amepongeza wakulima kuridhia kuuza korosho hizo huku akiwataka kujikita katika kilimo cha mazao mengine ya Biashara katika kipindi hiki msimu wa korosho ukielekea ukingoni.

Amewaomba wakulima kuridhia kufanyika kwa mnada wa tisa wiki mbili zijazo badala ya wiki ijayo, kutokana na uwepo wa korosho chache zinazopelekwa Maghalani.

Kwa upande wake Mohmedi Salumu na Juma salehe kasiki wakulima kutoka kata ya Mtawanya, wameiomba serikali kuangalia kwa jicho lingine kwenye zao la korosho kutokana na uwepo wa beii isiyoridhisha.

“Korosho inatumia gharama kubwa sana kuuza korosho Daraja la kwanza kwa shilingi 1,755/= na Daraja la pili 1,201/= au 1,000/= hairidhishi na haiinui uchumi wa mkulima”.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…