MWANDSIHI WETU, NEWALA

mtwarapressclub@gmail.com

Wakulima Wilayani Newala wahamasika kulima zao la ufuta baada ya kupewa mbegu bora kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI Naliendele huku kila kata ikipatiwa mbegu na kuwekwa shamba darasa.

Akizungumza katika shamba darasa la kata ya Nambali Wilayani Newala Afisa Kilimo wa Kata hiyo  Modestus Benedict amesema kuwa mashamba hayo yamekuwa sehemu ya hamasa ya kulima zao hilo.

“Hali ya mwaka huu ilikuwa na upungufu wa mvua hali lakini ufuta umeota tena mbegu zingine zimeonyesha kutoa hadi maua jambo ambalo linaonyesha kuwa tafiti zinafanyakazi ipasavyo.

“Mashamba haya yameletwa ili kuonyesha wakulima kuwa tunaweza kulima zao hili hukuhuku bila kwenda mbali ardhi inafaa kulima ufuta tumejaribu na tumedhibisha

Naye Afisa Kilimo Kata ya Chilangala Selemani Kamtande amesema kuwa wameanzisha shamba darasa la ufuta ili kutoa elimu kwa wakulima wa kata hiyo.

“Tunalo shamba darasa la ufuta ambalo tumelianzisha kwaajili ya kuwapa darasa wakulima tunapokea wageni wengi kuja kujifunza changamoto imekuwa hali ya hewa japo mbegu zimejitahidi kuvumilia ukame na magonjwa”

“Wakulima wanapaswa kuja na kujifunza hapa  tumelima pamoja na ukame lakini ufuta bado upo  unavumilia naimani kwao ni fundisho na hawataenda mbali na familia zao na unafanya vizuri zaidi”

Kwa upande  wake Mratibu wa Program ya zao la Ufuta Kitaifa Joseph Nzunda alisema kuwa mvua imekuwa changamoto kubwa kwenye ufuta mwaka huu.

“Tumeona kuna changamoto ya hali ya hewa mvua hazijanyesha kwa muda mrefu hali ya ufuta sio mbaya japo sio ilivyotegemewa wakulima walipanda kwa muda mzuri lakini hali ya hewa ikawa sio nzuri” alisema Nzunda

“Mbali na kuwepo kwa ukame lakini ufuta bado umeendelea kuwepo na kuvumilia ukame hili ndio lengo la watafiti kupata mbegu zinazovumilia magonjwa wadudu na zenye tija kwenye mavuno ambapo ufuta hustawi hata milimita ya mvua 400 hizi mbegu zinawafaa pia zinatumia muda mfupi”

Kitengo cha Uharishaji wa Teknologia na Uharishaji Gasper Mgimiloko alisema kuwa tunapita kuangalia mashamba ya mfano katika mkoa wa Mtwara ambapo tumeona ufuta umestawi vizuri na kuondoa dhana ya  wakulima kwenda kulima ufuta mbali.

Eneo hili lina Mwinuko usawa wa bahari ambao ni  mita 790 mpaka 805 pia kuna kabaridi kidogo ambapo tumeleta mbegu tatu mwishoni tutaangalia ipi imefanya vizuri na inaweza kuhimili mazingira ya huku” amesema Mgimiloko

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…