MWANDISHI WETU, MOROGORO

mtwarapressclub@gmail.com

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, ameeleza kuwa kiwango cha kufubaza VVU kimeendelea kukua na kufikia wastani wa asilimia 78%.

Waziri Mkuu amesema hayo Desema 1, 2023 wakati akizindua ripoti ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI, ambayo inaonesha maambukizi mapya miongoni mwa watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 15 yanaendelea kupungua nchini.

Uzinduzi wa ripoti hiyo, ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Morogoro, mjini Morogoro.

Akizungumzia kuhusua kiwango cha kufubaza VVU, Waziri Mkuu amesema ripoti ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI imeonesh kwa upande wa wanawake kiwango kimekua kwa asilimia 80.9 na wanaume asilimia 72.2 ikilinganishwa na asilimia 52 iliyokuwepo kulingana na utafiti wa mwaka 2016/2017.”

“Kiashiria hiki ni muhimu kwa sababu mtu anapokuwa amefubaza VVU anakuwa na afya njema na hatasumbuliwa na UKIMWI pamoja na magonjwa nyemelezi”

“Pia anapofikia kiwango ambacho virusi havionekani maabara, basi hataweza kuambukiza VVU kwa wengine,”

“Maambukizi mapya miongoni mwa watu wazima wenye zaidi ya miaka 15 yanaendelea kupungua kutoka watu 72,000 waliokuwepo mwaka 2016/2017 hadi watu 60,000 kwa mwaka 2022/2023”

Hii ni sawa na upungufu wa asilimia 0.18 ambapo asilimia 0.24 ni wanawake na asilimia 0.11 ni wanaume,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa

Ili kuendelea kupunguza maambukizi ya VVU, Waziri mkuu amewataka wadau mbalimbali kushirikiana na serikali huku akiwaomba viongozi wa dini, siasa na kimila kutumia majukwaa yao kuendelea kuzungumza na jamii juu ya kupambana na ugonjwa wa Ukimwi.

Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Morogoro, mjini Morogoro, huku mikoa na Wilaya mbalimbali nchini zikifanya pia maadhimisho hayo.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…