JUMA MOHAMED, MTWARA
mtwarapressclub@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda amewataka Madiwani na Watendaji wa Sekta ya Afya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, kutoa elimu ya afya ya uzazi ili kupunguza vifo kwa wanawake wajawazito na watoto wachanga.
Akizungumza Novemba 6, 2023 katika mkutano wa baraza la Madiwani wa kujadili taarifa za kwenye Kata robo ya kwanza uliofanyika katika ukumbi wa Boma wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Munkunda alisema kuwa Serikali imetumia fedha nyingi kuwekeza kwenye sekta ya afya lakini takwimu bado zinaonyesha kuna ongezeko kubwa la vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga.
Alibainisha kuwa wanawake wajawazito wengi Mtwara huwa hawahudhulii kliniki kwa wakati hivyo hubainika wanachangamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa damu katika hatua ya mwisho na kuongeza kuwa ni wakati sasa wa wakuu wa vituo vya afya na zahanati kutoa taarifa ya hivyo ili waweze kutafutia ufumbuzi.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka Madiwani hao kuhamasisha wananchi wa Mtwara kuzingatia kilimo cha mazao mchanganyiko hasa zao la mbaazi, choroko na korosho ambayo tayari soko la kitaifa lipo nchini India.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameomba ushirikiano kutoka kwa madiwani na watendaji ili aweze kutekeleza vema majukumu yake.
Takwimu za mkoa kupitia sekta ya afya zilizotolewa kwenye kikao cha Baraza la Ushauri la Mkoa (RCC) zimeonesha Mkoa wa Mtwara kuwa na vifo 17 kwa wajawaziyo, huku watoto wachanga 179 wakipoteza maisha ndani ya kipindi cha miezi Mitatu ya Julai hadi Septemba 2023.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






