BRYSON MSHANA, MTWARA
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania – TASAC, wameunga mkono juhudi za kuongeza ufanisi katika Bandari ya Mtwara, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Bandari maalum ya kusafirisha mizigo michafu.
Bandari hiyo maalum inatarajiwa kungwa eneo la Mgao Halmashauri ya Mtwara, lengo ikiwa ni kutenganisha usafirishaji wa mizigo misafi na michafu katika eneo moja linalotumika kwa sasa.
Wajumbe hao wa TASAC wamefanya mazungumzo na watendaji wa TPA, ambao wamewaeleza namna ambavyo wanasimamia na kuendesha shughuli mbalimbali za usafirisha wa mizigo na malengo ya kuongeza ufanisi ili kuwavutia wateja zaidi.
Akizungumza na waandishi wahabari katika eneo la Feri Novemba 7, 2023 baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Kapteni Mussah Mandia, ameipongeza TPA kwa mipango yake ikiwepo ujenzi wa Bandari maalum itakayojengwa eneo la mgao Mtwara DC, kwa ajili ya kusafirishia mizigo michafu.
Amesema Ujenzi huo wa Bandari ya Mgao utasaidia kuwa na eneo maalum la kusafirishia shehena za mizigo kama Makaa ya mawe, Saruji na madini mbalimbalimbali yanayotarajiwa kuanza kuchimbwa katika mikoa ya Mtwara na Lindi.
“TPA Mtwara wamejipanga vizuri, tayari wako kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa wanaimarisha eneo la usafirishaji ikiwa ni pamoja na kutenganisha bandari ili moja ihudumie mizigo misafi na nyuingine michafu, hii ni hatua kubwa na tunaipongeza” ameeleza Kapteni Mandia
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Udhibiti Ulinzi, Usalama wa Vyombo vya Majini na Mazingira ya Bahari kutoka TASAC Bi. Letisia Mutaki, amesema wanaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa meli zinazofanya shughuli mbalimbali zinazingatia sheria na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya usalama na utunzaji wa mazingira.
“Zipo taratibu zilizowekwa na zinafuatiliwa ili kuhakikisha kuwa watumaiji wanazifuata na ikibainika wapo wanaoenda kinyume huwa wanachukuliwa hatua kulingana na sheria za nchi zinazoongoza sekta ya usafirishaji wa majini” amesema Bi. Letisia Mutaki
Pamoja na kutembelea Bandari ya Mtwara, wajumbea hao pia walitembelea Mnara wa Masiliano ya Bahari uliopo eneo la Verani pamoja na kukagua maendeleo ya ukarabati wa Kivuko cha MV Kitunda kinachofanya safari zake eneo la kilambo Halmashauri ya Mtwara.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






