BRYSON MSHANA, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

+255 787 568 733

Machi 29, 2023 Tanzania ilipokea ugeni wa kihistoria kwa kutembelewa na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris akiwa katika ziara ya kumarisha ushikiano baina ya mataifa haya mawili ambao uliasisiwa zaidi ya miaka 60 iliyopita.

Kiongozi huyo alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ambao kwa pamoja walikutana na kufanya mazungumzo pamoja na kuafikiana juu ya ushirikiano wa mambo kadhaa ya maendeleo baina ya Tanznaia na Marekani.

Ushirikiano wa Tanzania na marekani ulianza mwaka 1961, na hatimaye mwaka 1968 nchi hizi mbili zilitiliana saini mikataba kadhaa ya ushirikiano ambayo hadi sasa uhusiano unazidi kuimarika zaidi.

Marekani ni miongoni mwa mataifa yanayofanya vizuri kwenye uwekzaji hapa nchini, ambapo hadi sasa miradi 226 ya Marekani imesajiliwa katika kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) ikiwa na thamani ya Dola 4.778 Bilioni na kuzalisha ajira 54,584 kwa watanzania. (Hii ni kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

Sambamba na hilo kuna ongezeko kubwa la idadi ya watalii wanaotoka Marekani ambao wameongezeka kutoka 66,394 mwaka 2015 hadi kufikia watalii 100,600 mwaka 2022.

Pamoja na kushirikiana karika sekta nyingine, Marekani na Tanzania ni washirika wakubwa katika biashara hasa katika Ukanda wa nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwa ni kati ya mataifa 136 yanayofanya biashara na Marekani na tangu kwa zaidi ya 50, ikikadiriwa kuwa jumla ya biashara za kuuza na kununua zinazozidi Dola 316 milioni.

Wakati wa ziara ya Kamala Harris, Tanzania na Marekani zilisaini baadhi ya hati za ushirikiano katika sekta za Bandari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na biashara.

Sambamba na kusainiwa kwa hati hizo, Rais Samia pia alikaribisha ushirikiano na Marekani katika maeneo ya uvuvi hasa katika bahari kuu, uvuvi wa samaki, uchimbaji wa chumvi, utafiti wa mafuta na gesi, utalii na usafirishaji wa baharini.

Rais Samia alikaribisha ushirikiano na Marekani katika maeneo ya uvuvi hasa katika bahari kuu, uvuvi wa samaki, uchimbaji wa chumvi, utafiti wa mafuta na gesi, utalii na usafirishaji wa baharini.

Pia alizungumzia suala la viza na kueleza kuwa Tanzania inakaribisha utayari wa Marekani kufanya mapitio ya mkataba wa viza ya sasa ili kuwezesha raia wa nchi hizo mbili kunufaika na viza ya muda mrefu.

Hayo yalikuwa yale ya kitaifa kwa ujumla, lakini Rais Dk. Samia alizungumza jambo lingine ambalo liligusa Bara la Afrika kwa ujumla, akiiomba Serikali ya Marekani kufanya marejeo ya mkataba wa Mpango wa Ukuzaji Fursa za Kiuchumi Afrika (African Growth and Opportunity Act – AGOA) na kuuhuisha hadi mwaka 2030.

Rais Samia alisema mpango wa AGOA ambao unaisha mwaka 2025 ni muhimu kwa Tanzania kwa kuwa ni njia pekee ya biashara ambayo bara la Afrika linautegemea kujikomboa kutoka lindi la umaskini.

Maombi haya ya Rais Samia, sio kwamba tu yanaihusu Tanzanaia lakini yanaihusu Afrika nzima ambayo ndiyo mlengwa mkuu wa mkataba huu, hivyo alichokifanya ni kulisemea Bara zima la Afrika kupitia fursa ya ziara ya Mkamu wa Rais wa Marekeni Nchini Tanzania.

Je Mkataba wa GOA ni rasmi?

Mkataba/Mpango huu wa AGOA upo kwa mujibu wa sheria na uliasisiwa Mei 18, 2000 na kutiwa saiani na aliyekuwa Rais wa Marekani, Bill Clinton,  ukikusaidia kuwezesha wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika ikiwamo Tanzania kuuza bidhaa, kukuza mitaji pamoja na kupanua masoko kiuchumi katika nchi ya Marekani.

Mkataba wa AGOA hutoa fursa na nafasi kwa mataifa ya Kiafrika kusafirisha bidhaa zinazokadiriwa kufikia 6,400 nchini Marekani bila kulipa ushuru, na unatarajiwa kufikia mwisho mwaka 2025, na kwa kuliona hilo ndio maana Rais Samia ameomba urefushwaji wake hadi mwaka 2030.

Faida za AGOA kwa Tanzania

Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazofaidika na mpango huo kwa kuuza bidhaa mbalimbali Marekani na hadi kufikia mwa 2010, mauzo ya bidhaa za Tanzania nchini Marekani yaliingiza Dola Milini 15 za marekani sawa na Shilingi Bilioni 24 za Tanznaia ikiwa ni zaidi ya asilimia 73.1 tangu kuasisiwa kwa AGOA.

Mwaka uliofuatia wa 2011, Marekani iliuza bidhaa zake Tanzania zenye thamani ya Dola 258 milioni, sawa na asilimia 57.7, ikiwa ni zaidi ya Dola 94 milioni tangu mwaka 2010, na zaidi ya asilimia 474.7 tangu mwaka 2000.

Kupitia mpango huo, Marekani pia ilinunua kutoka Tanzania mashine mbalimbali za gharama inayofikia Dola milioni 61, ngano Dola milioni 53 milioni, bidhaa za nguo Dola milioni 25, mpira Dola milioni 15, na mashine za umeme za Dola milioni 13.

Kwa mazao ya kilimo, Marekani ilinunua kahawa, viungo, chai zilizoliingizia taifa Dola 29 milioni, mbogamboga ziliingiza Dola 5 milioni, matunda, korosho Dola 2 milioni na kahawa iliyoingiza Dola 28 milioni.

Hiyo ni kwa upande wa Tanznia, lakini kwa mujibu wa taasisi ya kiuchumi ya Brookings, Afrika kusini mwaka wa 2019 iliingiza dola milioni 917 kutokana na mauzo ya magari na vifaa vya kilimo Marekani.

Kwa upande mwingine Utafiti tofauti uliyofanywa na chuo kikuu cha Afrika kusini mwaka wa 2017 unaonyesha kwamba Marekani iliagiza asilimia 10 ya mvinyo wake kutoka Afrika kusini kwa gharama ya dola milioni 59.

Ombi la Rais DK. Samia limekuja wakati muafaka

Rais Dk. Samia amewasilisha ombi la kurefushwa kwa mkataba wa AGOA wakati ambapo mataifa ya Afrika yanahitaji ushirikiano zaidi wa kibiashara nay ale ya Ulaya, Asia pamoja na Marekani.

Ni dhahiri kuwa moja ya mambo ambayo Makamu wa Rais wa Marekani atakuwa ameondoka nayo katika ziara yake ya mataifa kadhaa ya Afrika ni Ombi la kurefushwa kwa mkataba wa AGOA lililowasilishw ana Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DK. Samia Suluhu Hassan.

Ni hii ni kutokana na Marekani kuendelea kutamani kufanya kazi na Afrika, na hili limedhihiriwa pia na Rais wa Marekani wa sasa Joe Biden ambaye July 2021 alizindua programu inayolenga kufanya biashara na mataifa ya kiafrika kwa jina Prosper Africa Build Together, wakati ukiomba dola milioni 80 kutoka kwa bunge ili kufaulisha mradi huo.

Program ya Prosper Africa inalenga kuongeza viwango vya biashara kati ya Marekani na Afrika na itazidi kuipa nguvu ile ya AGOA inayopigiwa chapuo kuzogezwa hadi mwaka 2030.

Kulingana na Gerrishon Ikiara, ambaye ni mhadhiri wa masuala ya kiuchumi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, anasema kuwa mipango ya AGOA na Prosper Africa utaimarisha uhusiano kati ya Marekani na Afrika ikiwemo kuongeza muda wa mikataba tajwa.

Anasema kuwa lengo la Marekani ni kuimarisha uhusiano wa kiuchumi pamoja na kisiasa kwa kutumia umaarufu wake wa kimataifa, hivyo yanapokuja mawazo wazuri kama ya kurefusha mikata ya mashirikiano ya kibiashara lazima wayazingatie kwa manufaa ya pande zote mbili.

Kulingana na kile kinachoonekana katika utekelezaji wa makubaliano haya ya mkataba wa AGOA, tangu kusainiwa kwake zaidi ya miaka 20 iliyopita, ndio maana Rais Dk. Samia suluhu Hassana anaona umuhimu wa kurefushwa kwa mkataba huu ambao unamalizika 2025.

Ombi la Rais DK. Samia la kutaka marejeo ya mkataba wa AGOA na kurefushwa hadi mwaka 2020 halikuiangalia tu Tanzanaia wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani, bali lilizingati bara zima la Afrika.

Hata hivyo wakati ikisubiriwa hatma ya kurefusha muda wa mkataba huo, bado wafanyabiashara wa tanzania wanayo fursa ya kutumia kipindi kilichobaki kufikia 2025 ambao umechagizwa zaidi za ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani hapa nchini sambamba na mazungumzo baina yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia Dk. Samia suluhu Hassan.

Check Also

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…