RAMLA MASALI, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo amesema wapo watu wagombanishi na wachonganishi ambao kazi yao ni kuhamisha masuala ya msingi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwenda kwa mtu na kufanya Rais aneonekane nafanya mambo binafsi.

Chongolo amezungumza hayo leo Julai 16, 2023, katika mkutano wa hadhara kuzungumza na wannachi wa Kanda ya Kusini katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

“Watu hao wanatengeneza mazingira ya kuwagombanisha ninyi, Ilani yenu, pamoja na viongozi wenu waliopewa dhamana ya kuratibu utekelezaji wa Ilani. “ Amesema Chongolo.

Aidha amesema kuwa watu hao wanahoji mambo machache mengine awahoji kama ujenzi wa miundo mbinu ya Barabara.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…