BASHIRU  MOHAMED, MTWARA

Wakazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara wamepongeza  kampeni ya KITAA KIMEITIKA-TB INATIBIKA-CHUKUA HATUA kupitia Kliniki Tembezi inayotoa huduma za  uchunguzi wa ugonjwa wa Kifua Kikuu ambayo inafanyika bila malipo.

Zaidi ya wananchi 200  wamejitokeza,mkoani Mtwara kuja   kufanya uchunguzi wa ugonjwa wa Kifua Kikuu, zoezi ambalo limefanyika  katika kituo cha mabasi Mkanaledi  kilichopo Manispaa ya mtwara – Mikindani.

Wananchi hao wametoa pongezi wakieleza kuwa utaratibu huo umewasaidia kupunguza gharama za kwenda kituo cha afya kwa ajili ya kufanya uchunguzi, huku wakitoa wito kwa  wananchi wengine kujitokeza ili kupata huduma hiyo.

Kwa upande wake Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma mkoa wa Mtwara Dkt. Michael Koni amesema kuwa kampeni hiyo ina lengo la kumsadia mwananchi kupunguza gharama za kufanya uchunguzi  ambapo itafanyika kwa siku 14 katika halmashauri zote za mkoa wa Mtwara, huku malengo ni kuwafikia wagonjwa zaidi ya 800.

Kampeni hiyo imeratibiwa na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa kushirikiana na mradi wa USAID Afya Yangu Kanda ya Kusini Mtwara.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…