BRYSON MSHANA, MTWARA
Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mtwara Mjini, kimetangaza matokeo ya nafasi ya Ubunge Jimbo la Mtwara Mjini, kufuatia kura za maoni zilizopigwa tarehe 4 Agusti 2025.
Akitangaza matokeo hayo leo Agusti 05,2025 katika Ofisi cha Chama hicho, Katibu wa CCM Wilaya ya Mtwara Mjini Fadhili Urami Ukasha, amemtangaza mtia nia aliyeongoza katika uchaguzi huo kuwa ni Dkt.Joel Nanauka aliyepata jumla ya kura 2045.
Ukasha ameeleza kuwa nafasi ya pili imeshikwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ndugu Hassan Mtenga, aliyepata kura 1610, akifuatiwa na Ndugu Judith Nguli aliyepata kura 582.
Waliofuatia ni Ndugu Baisa Abdala Baisa aliyepata kura 146, na kufutiwa na Ndugu Zhia Adinani Ally aliyepata kura 95 na Ndugu Engatraud Edmund Mbemba akapata kura 46.
Kura za maoni katika ngazi ya Ubunge na Udiwani kwa Chama cha Mapinduzi zilipigwa kote nchini tarehe 8 Agusti 2025, na matokeo yamekuwa yakiendelea kutangazwa katika maeneo mbalimbali.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






