MWANDISHI WETU, MBEYA

mtwarapressclub@gmail.com

Wananchi wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, wametakiwa kufanya kilimo biashara katika zao la kakao ili kuinua uchumi wao kutokana na bei ya zao hilo kuzidi kuongezeka.

Ushauri huo umetolewa  Desemba 18,2023,  na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi  iliyolenga kuona maendeleo ya zao la biashara la kakao wilayani Kyela.

Naibu Waziri ameiomba Wizara ya Kilimo kupitia maafisa ugani kutoa elimu kwa wakulima, ili kuzalisha kibiashara zaidi kutokana na zao hilo kuwa na faida kubwa katika kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa Ujumla.

Aidha amezielekeza Taasisi za SIDO na TIRDO kufanya utafiti wa namna ya kuzalisha bidhaa ya ziada inayotokana na mbegu ya zao hiyo ikiwemo kuzalisha juisi na pombe ya kisasa.

Amesema kuwa ziara hiyo ina lengo la kuhakikisha Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara katika kilimo hususani wa zao hilo pamoja na kufurahishwa na mfumo wa stakabadhi ghalani na kupanda kwa bei ya zao la Kakao kutoka Sh 9,800 mpaka Sh10,000 kwa kilo moja.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Josephine Manase amewataka wananchi kulilimda zao la kakao pamoja na kuacha tabia ya kuuza kwa watu wakati, badala yake wafike katika minada inayotangazwa ili kuuza kwa bei elekezi inayotolewa.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Stakabadhi za Ghala Ndg.Asangye Bangua amewataka wakulima kuhakikisha wanapeleka kakao kwenye maghala ikiwa na ubora, ili kuzidi kuongezea thamani na uhakika wa soko.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…