MWANDISHI WETU, IRINGA
mtwarapressclub@gmail.com
Misitu Sports Bonanza kwa msimu wa 9, kwa Mwaka 2023,imefikia tamati Desember 16,2023 katika Viwanja vya Makao Makuu ya Shamba la Miti Saohill Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa,huku Timu ya Saohill Misitu ikiibuka na Ushindi baada ya kuichapa Timu ya Mgololo Misitu mikwaju ya penati 4- 3 katika mchezo huo.
Akizungumza Wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi mbalimbali kwa niaba ya Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti la Sao hill PCO Tebby Yoram, Mhifadhi Mwandamizi Peter Nyahende alisema bonanza hilo limeanza mwaka 2015 ambapo mpaka sasa wanamiaka Tisa tangu kuanzishwa kwa bonanza hilo.
Aidha Mhifadhi huyo amezitaja Timu ambazo zimeweza kushinda katika bonanza hilo kuwa Timu ya saohill misitu ambao wameshindia fedha taslimu sh 800,000 na Mshindi wa pili Timu ya Mgololo misitu ambapo ameshinda kiasi cha sh 600,000 huku Mshindi wa tatu ikiwa ni Timu ya Irundi misitu akijinuakulia sh 400,000.
Michezo mingine ambayo wameweza kupata zawadi kwenye bonanza hilo ni mbio ndefu na fupi, wanaume na Wanawake,kuvutia kamba ,Mchezo wa bao na Draft , kukimbia na maguni na volleyball pamoja na Mpira wa Pete.
Pia Nyahende ameeleza kuwa lengo kuu la michezo hiyo ni kuendelea kujenga uhusiano na jamii inayolizunguka shamba pamoja na kuifanya jamii kuwa sehemu ya shughuli za uhifadhi hasa za upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
” bonanza hili limekuwa linahamasisha na kuwaleta pamoja wananchi kushiriki kuhifadhi misitu namna ya utunzaji wa mazingira hivyo tunatarajia tunapokutana kwenye mabonanza kama haya ni kwa ajili ya michezo kwa sababu michezo ni furaha na inajenga afya pia.” Amesema Nyahende
Mashindano ya Saohill Misitu Sports bonanza huandaliwa na kudhaminiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania- (TFS) kupitia Shamba la Miti Saohill huku kauli mbiu ya mashindano haya kwa msimu wa 9 kuwa”Panda Miti kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi” ili kuweza kuhakmasisha wananchi kutumia vizuri msimu huu wa mvua kupanda miti katika maeneo yao.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






