MUSSA MTEPA, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Wananchi wa kata ya Msimbati Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara, wameeleza kufurahishwa na kitendo cha serikali kuwajengea kituo cha afya,kituo cha polisi na uwekaji taa za Barabarani kwenye vijiji vinavyopatikana katika kata hiyo.

Akizungumza baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini wa mikataba mitatu ya vituo hivyo Novemba 24,2023,  Farida Mohamedi Mjumpa mkazi wa kijiji  cha Mtandi kata ya Msimbati amesma ujenzi wa kituo cha Afya  itakuwa msaada kwa Wananchi wa eneo hilo kwani  hapo awali walikuwa wanapata shida kupata vipimo vya magonjwa  mbalimbali.

Aidha nae Hemedi Hassan mkazi wa Msimbati amesma kulikuwa na changamoto kubwa ya ukatikaji wa umeme hivyo kitendo cha serikali kutaka kuwainganisha na umeme unaozalishwa na  Kampuni ya M & P katika eneo hilo kutawaondolea hasara ya kuunguza vifaa vyao kutokana na ukatikaji wa umeme wa mara kwa mara.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mtwara Mwanahamisi Munkunda amemtaka mkurugenzi wa TPDC kuhakikisha miradi hiyo inaanza mara moja huku akimtaka itekelezwe ndani ya miezi mitatu iwe inekamilika.

Naye Mkurugenzi Mtendaji waa shirika la Maendeleo ya petroli nchini (TPDC) Mussa Makame,  amesema kuwa gharama za miradi hiyo mitatu ni shilingi Bilioni 1.426.

Sambamba na hilo mkurugenzi Mtendaji amekiri kuwa utaratibu uliokuwa unatumika hapo awali wa kuwatafuta Wenyeviti wa vijiji kuwapatia mahitaji yao haukuwa mzuri hivyo kupitia ziara ya Naibu waziri mkuu na Waziri Wa Nishati Dk. Dotto Biteko wanaenda kuwa na uataratibu mpya utakaoleta tija.

Ameutaja utaratibu huo kuwa ni kuwepo maafisa Maendeleo ya jamii na maafisa Uhusiano  ambao wapangwa katika maeneo ya Msimbati na Madimba ili kuwarahisishia wananchi na shirika kupata taarifa zao.

Haya ni Matokeo ya Ziara iliyofanywa hivi karibuni na Naibu waziri mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko ambapo akiwa eneo la Msimbati tarehe 14 Novemba, 2023 aliitaka TPDC na Halmshauri kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa kata ya Msimbati na Madimba.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…