BRYSON MSHANA, MTWARA
Chama Kikuu cha Ushirika MAMCU Ltd kinachohudumia Wilaya za Nanyumbu, Masasi na Mtwara kimeuza zaidi ya Tani Elfu 50 za Korosho katika minada mitano ya awali huku kiasi cha fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kikiwa kimeshalipwa kwa wakulima.
Akisoma taarifa ya mwenendo wa minada katika mnada wa sita wa Korosho uliofanyika katika Kijiji cha Madimba Wilaya ya Mtwara Novemba 24, 2023, Meneja wa MAMCU Bi Biadia Matipa ameeleza kuwa wakulima wanaendelea kulipwa fedha zao kupitia vyama vyao vya msingi.
Ameseam kuwa jumla ya kilo 51,962,715.30 ambazo ni wastani wa Tani Elfu 51.9 ambazo zimekusanywa kutoka katika maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na Chama Kikuu MMACU zilishauzwa, na wakulima wanaendele kukusanya Korosho kwa ajili ya kuziuza katika minada inayofuata.
Katika mnada wa sita Novemba 24, 2023, kilo 6,696,616 sawa na Tani 6,696 za Korosho zilipelekwa mnadani huku wanunuzi 31 wakijitokeza kuomba kununua ambapo wakulima walikubali kuuza kwa bei ya kati ya shilingi 1,840 na 1,700.
Wakulima hao walikubaliana kuwa kiasi cha kilo 2,172, 615 ambacho wanunuzi waliweka bei ya shilingi 1,700, kibakishwe maghalani na kupelekwa kuuzwa katika mnada ujao.
Mwenyekiti wa MAMCU Siraji Mtenguka, amewaeleza wakulima kuwa kiasi cha tani elfu 2.1 kilichobaki kitaendelea kutafutiwa wanunuzi ambao watafikia bei ya kuanzia shilingi 1,700.
“Nawashauri wakulima wenzangu tuuze korosho zetu kwa bei ya shilingi 1,700 kwenda juu na sio chini ya hapo, zile zinazobaki ziendelee kutunzwa kwa ajili yam nada ujao au kama akipatikana mnunuzi wa kufika bei atauziwa” ameseam Siraji
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






