BRYSON MSHANA, MASASI

mtwarapressclub@gmail.com

Wakulima wa zao la Korosho  Wilayani Masasi mkoani Mtwara, wameuza Jumla ya Tani Elfu 9.4 za Korosho kwenye Mnada wa tatu  uliosimamiwa na Chama Kikuu chu Ushirika MAMCU Ltd, uliofanyika Novemba 03, 2023 katika Kijiji cha Mpindimbi Hamashauri ya Masasi.

Katika mnada huo ambao Serikali iliwawakilishwa na mkuu wa Wilaya ya Masasi Laurent John kanoni ,jumla ya  Kampuni 46 zilijitokeza na ziliwasiisha maombi ya kununua Korosho katika Maghala mbalimbali yaliyopo Masasi, Nanyumbu na Mtwara.

Kiasi ya bei ya Juu iliyofikiwa na wanunuzi katika mnada huo ilikuwa Shiingi 2,135 na bei ya chini shilingi 1,950 hali iliyoashiriria kuwa na ongezeko la bei ikilinganishwa na minada miwili liyopita ambapo katika mnada wa kwanza bei ya juu ilikuwa Shilingi 2,031/= na mnada wa pili Shilingi 2,070/=.

Kwa upande wa bei ya chini mnada wa kwanza ilikuwa shilingi 1,900 na mnada wa pili ikafikia Shilingi 1,920/= hali inayoonesha kuwa kuna kuimarika kwa bei za Korosho tangu kuanza kwa msimu 2023/2024 Octoba 20, 2023.

Akitoa salam za Serikali kwa wakulima wa korosho wa Kijiji cha Mpindimbi waliojitokeza kwenye mnada huo, Mkuu wa wilaya ya Masasi Laurent kanoni amewataka wakulima kutumia vizuri mapato yanayotokana na kuuza Korosho ili yawasadie katika mambo mengine ya maendeleo.

Amewaeleza wakulima hao kuwa wanao wajibu wa kuangalia matumizi mengine yaliyopo mbele yao ikiwepo kununua vyakula, kusomesha watoto pamoja na kuandaa mashamba kwa ajili ya mazao mengine yakiwepo yale ya chakula.

“Nimesikia hapa kuwa tayari wanunuzi wameshaanza kulipa fedha kwa vyama vya ushirika, mkatumie fedha hizo vizuri ili ziwasaidie kununua vyakula, na kuwaandaa watoto waliomaliza dara la saba kwa ajili ya kujiunga na kidato cha kwanza mapema mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2024”

“Vile vile niwasisitize juu ya kuendelea na kilimo cha mazao mengine ya chakula ili kujipatia akiba ya kutosha ya chakula, lakini msisahu pia kilimo cha mazao mengine ya biashara kama ufuta na Mbaazi ambayo yanakubali katika ardhi ya maeneo yetu mengi” amesisitiza DC Kanoni

Mwenyekiti wa MAMCU Siraji Mtenguka,  amesema bei ya mnada huo wa tatu ni ya kuridhisha kwani imepanda ilinganishwa na minada ya awali, na kusisitiza kuwa yeye akiwa muwakilishi wa Wakulima anaendelea kuwasiliana na mamlaka zingine kwa ajili ya kupata uhalisia wa bei ulivyo duniani.

“Wakulima wameshuhudia bei ikipanda kidogo, hii ni ishara nzuri na ndio maana wameridhia kuuza korosho zao wakiamini kuwa juhudi zinaendelea kufanyika ili waendelee kupata bei nzuri zaidi katika minada inayofuata” ameeleza Siraji.

Check Also

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…