BRYSON MSHANA, MASASI
mtwarapressclub@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Laurent John kanoni, amewashauri wakulima kuzingatia kununua mahitaji ya muhimu wakati huu ambao wameanza kupata malipo yatokanayo na Korosho wanazoendelea kuuza kwa wanunuzi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ametoa ushauri huo Novemba Novemba 03, 2023, wakati akiwasilisha salaam za Serikali kwa wakulima wa korosho wa Kijiji cha Mpindimbi Halamshauri ya Masasi, waliojitokeza kushuhudia mnada wa tatu uliandaliwa na Chama kikuu cha Ushirika MAMCU.
Amewashauri wakulima hao kutumia vizuri mapato watakayoyapata baada ya kuuza Korosho za msimu huu wa 2023/2024 ili yawasadie kufanya mambo ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi midogo itakayowasaidia kuongeza kipato.
“Ndugu zangu leo natoa salaam tu na nitakuja wakati mwingine kwa ziara rasmi ili tuzungumze zaidi, lakini leo niwakumbushe juu ya kuhakikisha kuwa mapato tunayoendelea kuyapata baada ya kuanza kuuza kurosho tuyaelekeze kwenye kujiendeleza kiuchumi”
““Nimesikia hapa kuwa tayari wanunuzi wameshaanza kulipa fedha kwa vyama vya ushirika, mkatumie fedha hizo vizuri ili ziwasaidie kununua vyakula, na kuwaandaa watoto waliomaliza dara la saba kwa ajili ya kujiunga na kidato cha kwanza mapema mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2024”
“Vile vile niwasisitize juu ya kuendelea na kilimo cha mazao mengine ya chakula ili kujipatia akiba ya kutosha ya chakula, lakini msisahu pia kilimo cha mazao mengine ya biashara kama ufuta na Mbaazi ambayo yanakubali katika ardhi ya maeneo yetu mengi” amesisitiza DC Kanoni
Katika mnada huo uliosimamiwa na Chama Kikuu chu Ushirika MAMCU Ltd, wakulima hao waliridhia kuuza Juma ya Tani Elfu 9.4/= kwa bei ya kati ya Shiingi 2,135 na 1,950/= ambapo jumla ya Kampuni 46 ziliwasiisha maombi ya kununua Korosho katika Maghala mbalimbali yaliyopo Masasi, Nanyumbu na Mtwara.
Bei hizo za mnada wa tatu, zimeonesha ongezeko la bei ikilinganishwa na minada miwili liyopita ambapo katika mnada wa kwanza bei ya juu ilikuwa Shilingi 2,031/= na mnada wa pili Shilingi 2,070/=.
Kwa upande wa bei ya chini mnada wa kwanza ilikuwa shilingi 1,900 na mnada wa pili ikafikia Shilingi 1,920/= hali inayoonesha kuwa kuna kuimarika kwa bei za Korosho tangu kuanza kwa msimu 2023/2024 Octoba 20, 2023.
Mwenyekiti wa MAMCU Siraji Mtenguka, alieleza kuwa bei ya mnada huo wa tatu ni ya kuridhisha kwani imepanda ilinganishwa na minada ya awali, na kusisitiza kuwa yeye akiwa muwakilishi wa Wakulima anaendelea kuwasiliana na mamlaka zingine kwa ajili ya kupata uhalisia wa bei ulivyo duniani.
“Wakulima wameshuhudia bei ikipanda kidogo, hii ni ishara nzuri na ndio maana wameridhia kuuza korosho zao wakiamini kuwa juhudi zinaendelea kufanyika ili waendelee kupata bei nzuri zaidi katika minada inayofuata” ameeleza Siraji.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…






