JUMA MOHAMED, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Benki ya NMB imezindua kampeni ya Bonge la Mpango, Mchongo wa Kilimo msimu wa Pili, maalumu kwa ajili ya wakulima wa zao la Korosho Kanda ya Kusini, ambapo kwa wiki Tano wakulima watajishindia Pikipiki Moja na fedha taslimu.

Kampeni hiyo imezinduliwa leo Novemba 02, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas, ambaye amewataka wakulima kutohifadhi ndani fedha zao, na baadala yake watumie taasisi za kifedha.

“Wapo watu nyumba inaungua unamuona analia anagalagala kwenye vumbi, unafikiria kinachomliza ni bati yake na madirisha ya nyuma yake kuumgua moto, kumbe wengine wanalia chini ya uvungu wa vitanda vyao kumejaa ndoo za fedha.”

“Sasa ili vilio vile viwe vifupi viwe vichache vya kulilia bati basi niwasihi tuwe na utamaduni wa kutunza fedha zetu kwenye mabenki.” Amesema Kanali Abbas.

Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kusini Faraja Ng’ingo akaeleza juu ya utaratibu wa kichezesha droo za Bonge la Mpango, ambapo kila wiki atapatikana mshindi mmoja wa Pikipiki na mmoja wa fedha taslimu shilingi 100,000, kwa muda wa wiki Tano.

Katika droo ambayo imechezeshwa kupitia uzinduzi huo, mkazi wa wilaya ya Newala ndugu Said Likumbea ameshijishindia Pikipiki moja aina ya TVS.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…