BRYSON MSHANA
Mtwarapressclub@gmail.com
Taarifa iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania leo Octoba 31, 2023 imeeleza kuwa Pato la Taifa kwa Tanzania Bara lilikua kwa kiwango cha kuridhisha cha asilimia 5.4 na asilimia 5.2 katika robo ya kwanza na ya pili, na kuna matarajio ya kufikia makadirio ya ukuaji wa asilimia 5.3 kwa mwaka 2023.
Kwa upande wa Zanzibar, taarifa hiyo imesema uchumi ulikua kwa asilimia 6.2 katika robo ya kwanza ya 2023, na kuna uwezekano mkubwa wa kufikiwa kwa lengo la ukuaji wa asilimia 7.1 kwa mwaka 2023
Hayo ni kwa mujibu wa Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ya Benki Kuu ilifanya mkutano wake wa 228 tarehe 27 Oktoba 2023, uliolenga kutathmini utekelezaji wa sera ya fedha na mwenendo na mwelekeo wa uchumi.
Kupitia Mkutano huo, kamati ilibaini kuwa utekelezaji wa sera ya fedha ulichangia kuwepo kwa kiasi cha kutosha cha ukwasi kwenye uchumi kwa mwezi Agosti, Septemba na Oktoba 2023.
Kamati hiyo pia ilitathmini mwenendo wa uchumi wa dunia kwa mwaka 2023 na kubaini kuwa, uchumi wa dunia bado haujaimarika licha ya ukuaji wa juu ya matarajio uliofikiwa katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka.
Kulingana na kamati, mwenendo huo unatokana na kubanwa kwa sera ya fedha katika nchi nyingi duniani, migogoro ya kisiasa na ongezeko la bei za mafuta.
Kamati imeeleza kuwa mfumuko wa bei umepungua kutoka viwango vilivyofikiwa mwaka 2022, licha ya kubakia juu ya malengo kwa nchi nyingi.
Taarifa imeeleza kuwa Mfumuko wa bei kwa Tanzania Bara umepungua na kufikia asilimia 3.3 mwezi Septemba 2023, kutoka asilimia 3.6 mwezi Juni 2023, ukichangiwa na kupungua kwa bei za vyakula.
Kwa upande wa Zanzibar, mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 7.5 ukilinganisha na asilimia 6.5 mwezi June 2023.
SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI
Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika…






