GREGORY MILANZI, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Mkoa wa Mtwara umezindua Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (PJT-MMMAM), program inalenga maeneo makuu 5 ambayo ni Afya bora,lishe, Malezi yenye mwitikio, Fursa za ujifunzaji wa awali na Ulinzi na usalama kwa watoto kuanzia umri wa miaka 0 mpaka 8.

 Akizindua program hiyo tarehe 5 Septemba 2023, Mgeni rasmi mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abasi amesema wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wanatakiwa kuhakikisha wanakabiliana na tatizo la udumavu, kuwapa huduma bora za malezi ya awali na program za elimu ambazo zitawezesha kukua na kufikia ukuaji timilifu.

Kanali Ahmed Abasi amesema kuwa,kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ofisi ya Takwimu ya Taifa mwaka 2021/2022, tatizo la hali duni ya lishe limebainika kupungua kwa baadhi ya viashiria kwa watoto chini ya miaka 5 ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2018/2019.

Ameongeza kuwa Mkoa wa Mtwara tatizo la udumavu limepungua kutoka watoto 57,600(29.6%) hadi watoto 42,460(22%) wakati tatizo la uzito pungufulimepungua kutoka watoto 18,240(11.5%) hadi watoto 11,540(6%), sambamba na hilo tatizo la uzito mkubwa wa mwili limebainishwa kupungua kutoka watoto 7,680 (4%) hadi watoto 3,840 (2%).

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, mkoa wa Mtwara una idadi ya watoto wapatao 349,639 (wavulana 173,991 na wasichana 175,648) wenye umri wa miaka 0-8 ambao ni sawa na asilimia 21.4 ya watu wote. Hii inamaanisha kuwa katika kila watu wane kuna mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 0-8.

Afisa maendeleo ya Jamii kutoka Waizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na makundi maalum Salome Francis amesema program hii ikitekelezwa kama ilivyopangwa, italeta matokeo chanya kwa watoto wa umri wa miaka 0-8, pia amewaomba wananchi kuhakikisha utekelezaji unafanyika katika ngazi ya halmashauri na jamii na kuhakikisha wazazi, walezi na Jamii kwa ujumla ili kuweza kuwapa watoto elimu jumuishi ya mradi.

Mwakilishi wa Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Children in Crossfire Davis Gisuka amesema kuwa mtoto ana uwezo mkubwa sana wakujifunza akiwa na umri wa miaka 0 mapa 3 maana ubongo wake unakuwa tayari kwajili yakujifunza mabo mbalimbali, ameomba Jamii kuhakikisha  wanawapa watoto fursa za ujifunzaji wa awali.

Mradi wa Programu jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) unatekelezwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na Makundi Maalum, Mtandao wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Tanzania (TECDEN), Umoja wa vyama vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Children in cross fire ( CIC) Kitovu cha Maendeleo safi (KIMAS).

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…