SILIVIA ERNEST, MBINGA

mtwarapressclub@gmail.com

Kaimu Mkuu wa Idara ya Viwanda, Bishara na Uwekezaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Bi. Martina Ernest Ngahi ametoa wito kwa wawekezaji waliopo ndani na nje ya Mkoa wa Ruvuma kuja kuwekeza katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Bi. Martina ametoa wito huo  tarehe 2 Septemba 2023, wakati akizungumza katika kipindi cha MBINGA YETU kinachorushwa na Radio Hekima iliyopo katika Wilaya ya Mbinga Mkoai Rvuma.

Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ina maeneo na fursa nyingi za kichumi hivyo ambazo zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo nchini.

” Katika Halmashauri yetu tuna fursa mbalimbali za kiuchumi mfano uwekezaji wa usindikaji wa sembe au zao la soya, ujenzi wa mahoteli na nyumba za kulala wageni na kadhalika” Amesema Bi. Martina

Aidha Bi. Martina amewakumbusha wafanya biashara waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuwa wabunifu na kutumia changamoto zilizopo kama fursa katika kuanzisha au kuimarisha biashara zao.

Amesema ” Ukiwa mfanya biashara lazima uwe mbunifu sio unaiga kila biashara jitahidi kupambania na kwenda nje ya boksi”

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…