MWANDISHI WETU, MTWARA

mtwarapressclub@gmail.com

Wakaguzi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara wametakiwa kuwatumikia wananchi ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za kiusalama zinazowakabili katika maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa na ACP-MTAKI.N.KURWIJILA ambaye alimuakilisha kamanda wa  Polisi Mkoa wa Mtwara N.S.KATEMBO-ACP katika kufunga mafunzo ya utayari awamu ya pili yaliyo hitimishwa tarehe 06.09.2023 katika Viwanja vya Polisi Mtwara.

ACP-KURWIJILA, amewataka Wakaguzi waliohitimu kwenda kutendea kazi yale yote ambayo wamejifunza katika mafunzo ya utayari kwa kipindi cha mienzi miwili.

Amesisitiza juu ya wahitimu hao kuhakikisha kuwa wanatumia elimu waliyoipata kuwahudumia vyema wananchi katika jamii kwenye maeneo yao, ili kuleta sifa njema kwa Jeshi la Polisi katika kutatua Changamoto zinazowakabili wananchi kwa wakati.

Mafunzo hayo yalikuwa ni ya muda wa mienzi miwili yakiwa na lengo la kuwasaidia wakaguzi kuongeza uweledi na ufanisi zaidi katika kutekeleza majukumu ya ndani na nje ya jeshi la Polisi.

Jumla ya Askari waliohitimu mafunzo hayo  ni 50 kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara, kati yao Wakaguzi wa Kike wakiwa ni 08, ambao walijumuika pamoja katika kipindi chote cha mafunzo yaliyohusisha masomo mbalimbali yakiwepo ya Darasani, Uwanjani na Medani za Kivita.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…