BRYSON MSHANA, TABORA

mtwarapressclub@gmail.com

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Elimu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwl. Vicent Kayombo akigawa vifaa kwaajili ya kufundishia somo la michezo kwenye shule 56 za Sekondari vilivyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la sports Development Aid (SDA).

Vifaa hivyo vilivyotolewa na SDA ni pamoja na mipira 504, Filimbi 112 na koni 1,008 vilivyogharimu shilingi Milioni 24.9

Shirika hilo la SDA limekuwa linajishughulisha na ukuzaji wa mandeleo ya elimu kwa vijana kupitia somo la michezo.

Zoezi hilo limefanyika Tarehe 25 June 2023, wakati wa shughuli ya ufungaji wa mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA 2023) yaliyofanyika kitaifa Mkoani Tabora.

Check Also

WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE

MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…