MWANDISHI WETU, LINDI
mtwarapressclub@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amezindua rasmi Maonesho ya Madini na Uwekezaji kwa lengo la kuongeza fursa za kiuchumi kwa wananchi wa mkoa huo.
Telack amezindua maonesho hayo kwenye kikao cha wadau wa madini kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Tarehe 0 Julai 2023.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mhe. Telack amesema kuwa Maonesho haya yanafanyika maalum Kwa ajili ya kutangaza fursa za madini zilizopo Mkoani Lindi ikiwemo dhahabu yenye ubora wa juu, graphite, gypsum, manganese,nickel, marble, Vito, Safaya na madini mengine isipokuwa Tanzanite na Almasi.
Telack ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa fursa za madini, Mkoa wa Lindi una fursa za uwekezaji kwenye kilimo, fukwe nzuri za bahari, utalii, uchakataji wa mazao hasa korosho na ufuta.
Kupitia kikao hicho, Telack amewakaribisha wadau wote kwenye sekta ya biashara, Viwanda, madini na sekta zote za uchumi kushiriki kwenye Maonesho ya Madini na Uwekezaji yatakayofanyika Wilayani Ruangwa kuanzia tarehe 21-26 Agosti 2023.
WANANCHI WA MABOGINI WANUFAIKA NA MRADI WA RISE
MOSHI-KILIMANJARO Wananchi wa kijiji cha Mabogini, kata ya Mabogini, wilayani Moshi Mkoani…







